Mwanasiasa Victory Ogeto Swanya amewaomba wahisani wema kusaidia shule za enoe hilo kwa kuwawekea umeme. 

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akiongea siku ya Jumapili katika shule ya msingi ya Nyanchonari, Wadi ya Nyakoba eneo bunge la Kitutu Masaba, alipozuru na kukutana na wasimamizi na walimu wa shule hiyo, mwanasiasa huyo aliwaomba wahisani wema kusaidia shule zote za eneo hilo kwa kuwaunganishia umeme kama njia moja ya kuinua viwango vya elimu.

Kulingana na Ogeto, mradi wa serikali wa kuweka umeme katika shule uliweka umeme katika baadhi ya madarasa huku wazazi wakigaramia madarasa mengine. 

Kwa sasa amewaomba wahisani hao kujitokeza na kusaidia wazazi kwani wazazi huwa na majukumu mengi ya kufanya. 

"Naomba wahisani na wasamaria wema kuwasaidia wazazi ili kuinua viwango vya masomo," alisema Ogeto. 

Kwingineko, aliwahimiza wanafunzi kutia bidii katika masomo ili waweze kujizolea alama bora katika mithiani yao.