Gavana wa kaunti ya Kisii James Ongwae ameagiza maafisa wa idara ya afya katika kaunti hiyo kuzipitia stakabadhi zote 90 za wahudumu wa afya katika kaunti hiyo ambazo walipokezwa kutathmini wale watapandishwa vyeo kwanzia mwezi wa tisa.
Wahudumu wa afya katika kaunti hiyo waliahidiwa kuwa yeyote amefanya kazi ya matibabu kwa zaidi ya miaka mitatu atapandishwa cheo na kuongezewa mshahara, jambo ambalo limeonekana kuafikiwa sasa baada ya wale wamehudumu miaka mitatu kuwasilisha stakabadhi zao kwa ofisi ya idara ya afya.
Mnaomo siku ya Jumanne, Karani wa kaunti ya Kisii Johnston Ngege alisoma ripoti hiyo ya gavana Ongwae afini mwake, huku ikibainika kuwa Ongwae anahitaji wahudumu wale wamedumu zaidi ya miaka mitatu kupandishwa cheo na kuongezwa mshahara.
Kwanzia mwenzi wa tisa, maafisa hao wataanza kupokezwa mshahara tofauti na kuwa katika vyeo tofauti ikiwa mpango huo utakamilika baada ya stakabadhi zao kupitiwa.
“Natumai wale wamefanya kazi katika sekta ya afya wataanza kupata mshahara mpya kwanzia mwezi ujao na kupandishwa vyeo,” ilisoma sehemu ya ripoti ya gavana Ongwae