Wahudumu wa pikipiki eneo la Kisauni wamekashifu mauaji ya mmoja wao siku ya Jumanne.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho, kijana huyo alipigwa risasi baada ya kuhusishwa na kundi la vijana linalowahangaisha wenyeji nyakati za usiku katika eneo hilo.

Wakizungumza siki ya Jumanne katika mazishi ya kijana huyo, wahudumu hao wa pikipiki walisema kwamba japo kijana huyo alikuwa akitafutwa na maafisa wa usalama, alikuwa na haki ya kukamatwa na kufikishwa mahakamani ili kujitetea.

Wakaazi hao walitaja mauaji hayo kama kitendo cha kinyama kwa madai kuwa alipigwa risasi wakati wa mchana huku wakaazi wa eneo hilo wakishuhudia.

Mohamed Abdi, ambaye aliwaongoza wenzake katika kugharamia mazishi ya kijana huyo, alisema kwamba ipo haja ya maafisa wa usalama kuwakamata wanaotekeleza visa vya uhalifu na wala sio kuwaua mbele ya wakaazi.

Tukio hili linajiri siku kadhaa tu baada ya Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Maalim Mohammed kuapa kukabiliana na visa vya uhalifu katika kaunti hiyo.

Eneo la Kisauni limetajwa kuwa makaazi ya kundi la uhalifu la Wakali Kwanza.