Wahudumu wa bodaboda kwenye mji wa kisii wameombwa kuzingatia sheria za barabara na kutopita sehemeu ambazo wamekatazwa.
Akiongea afisini mwake waziri wa barabara na ujensi kwenye kauti ya kisii, John Fredrick Omwoyo amewataka wahudumu wa bodaboda kutumia barabara walizotengewa na kaunti.
“Nawaomba wahudumu wa pikipiki kutumia njia walizotengewa,” alisema Omwoyo.
Ameongezea kuwa hii ni njia mojawapo ya kupunguza msongamano katikati mwa mji wa kisii.
“Hii ni njia moja ya kupunguza msongamano wa magari na pikipiki ambao umekuwa donda ndugu kwa mda mrefu,” aliongezea Omwoyo.
Vilevile amesema kuwa wale wahudumu watakaopatikana wakikaidi sheria hiyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
“Ni ombi kwa wahudumu wote wa bodaboda kutii sheria na wale watakaopatikana wakikaidi hii sheria watachukuliwa hatua kali za kisheria,” alionya Omwoyo.
Halikadhalika amesema kuwa kuna mikakati mahususi ya kuboresha usafiri kwenye mji wa kisii ambayo imeanza kutelezwa.
Ni siku za hivi punde ambapo vizuizi vimewekwa kwenye baadhi ya barabara mjini kisii na serikali ya kauniti ya kisii kama njia moja ya kupunguza msongamano wa magari na pikipiki ili kurahisisha usafiri.