Hoteli ya Mombasa Beach. [Picha/ tripadvisor.co.uk]
Wahudumu wa Hoteli ya Mombasa Beach wamesusia kazi kwa madai ya kucheleweshwa kwa mishahara yao ya miezi mitatu.
Wengi wa wahudumu hao wamelaumu mkurugenzi mkuu wa hoteli hiyo kwa masaibu yao.
Mkurungenzi huyo, Victor Shitaka, alijiunga na hoteli hiyo mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka uliopita.
Wakiongozwa na Adlin Kanana, wafanyikazi hao walilaumu uongozi wa hoteli hiyo kwa kuwakandamiza.
“Tunakandamizwa kwa kuwa hatupewi haki yetu kama katiba inavyosema,” alisema Kanana.
Mgomo huo umesababisha kulemazwa kwa shughuli za kawaida katika hoteli hiyo.
Kwa upande wake, Shitaka amewataka wafanyikazi hao kutokuwa na hofu na kuwahakikishia kuwa watapokea mishahara yao hivi karibuni.
“Musiwe na hofu yoyote kwani mutalipwa pesa zenu zote,” aliseam Shitaka.