Wakaazi wa eneo la Nyabite wilayani Nyamira kaunti ya Nyamira wamewaomba wahudumu wa kampuni ya nguvu za umeme (KPLC) katika kaunti hiyo kuwa maakini wanapounganisha nyaya za stima kuwaepusha kutokana na hatari za umeme.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wito huo umetolewa baada ya watu watano waliokuwa katika duka moja siku ya jumanne kunusurika kifo katika eneo hilo la Nyabite pale nyaya ya stima ilikatika na kuanguka kisha ikalipuka lakini hapakuwa na majeruhi.

Wakizungumza katika eneo hilo baada ya kisa hicho kutendeka wakaazi hao wakiongozwa na Peter Ochoke na Orina Mose walisema watano hao wangefariki papo hapo lakini walinusurika kwa kutoroka.

Kulingana nao licha ya kuwa maafisa wa kampuni hiyo waliunganisha nyaya hiyo siku ya Jumatatu juma hili bado ilichujuka siku moja tu baada ya ukarabati, hivyo wameomba kampuni ya KPLC kuwa maakini katika kazi yao.

“Hawa maafisa wa kampuni ya KPLC waliunganisha nyaya hii ya stima siku ya Jumatatu na leo ilikatika na kuanguka nusura wakaazi walio kuwa karibu hapa wafe tunawaomba wanapofanya kazi yao wawe maakini sana,” alisema Ochoke.