Wahudumu wa matatu katika kaunti ya Kisii wamekashifu kitendo cha na maafisa wa usalama waliokuwa wanaweka usalama katika mji wa Kisii kwa kumuua dereva mmoja.
Akiongea katika kituo cha matatu cha Keroka, mwenyekiti wa wahudumu hao Victor Manoti amekashifu kitendo hicho cha maafisa hao kwa kumpiga risasa dereva mmoja ambaye alikufa akiendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kibnafsi ya Ram.
“Nimekashifu kitendo hiki kilichotokea hii leo wakati polisi walimpiga risasi mmoja wa dereva wetu na ambaye ametuaga,” alihoji Manoti.
Dereva huyo alipigwa risasa katika kituo cha magari yanayopanga kuelekea Keroka-sotiki nyuma ya duka la jumla la Tuskys, baada ya kutaka kuwafurusha wanafunzi pamoja na wanabodaboda waliokuwa wanawarusha maafisa hao mawe kilichopelekea maafisa hao kufiatua risasi.
Wahudumu hao wamewakashifu maafisa hao kwa kuingia hadi kwa kituo hicho cha magari, ambapo kulikuwa na watu wenngi wakiwemo wasafiri ambao walihofyia maisha yao zaidi wakati dereva huyo aliuawa.
“Maafisa hawa wa polisi wamefanya kitendo cha unyama kwetu kama wahudumu wa magari kwa kuwa hatukutarajia waingie hadi hapa ndani na kusababisha maafa haya,” alihoji Josphet Onsase, dereva katika kituo hicho.
Kwingineko, wahudumu wengine walipata majeraha mabaya, haswa walipokuwa wakitoroka wakati mwenzao alipigwa risasi.
Kwa sasa wahudumu hao wamehapa kuelekea mahakamani ili kuwashtaki maafisa hao, hasa yule aliyempiga na kumuua dereva huyo ili haki itendeke, na kuomba kuwa mali yaliyoharibiwa serikali igharamie.