Share news tips with us here at Hivisasa

Wahudumu wa magari mjini Kisii wameoimba serikali kuweka matuta kwa barabara zote zinazoingia katika kituo cha magari mjini humo ili kuzuia visa vya kugongana kwa magari na kusababisha ajali.

Kulingana na wahudumu hao, gari nyingi zimekuwa zikihusika kwa visa vya ajali zinapoingia katika kituo hicho kwa kile kilichosemekana kung’ang’ania nafasi ya kupanga abiria.

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Ijumaa katika kituo hicho mjini Kisii, wahudumu wa magari mjini humo wakiongozwa na mwendeshaji gari Cleophas Ong’era waliomba serikali kuwawekea matuta kwa barabara hizo zote zinazoingia kwa kituo hicho ili kuzuia uendeshaji wa magari kwa kasi.

“Tumekuwa tukishuhudia ajali nyingi hapa kituoni Kisii maana gari nyingi huendeshwa kwa kasi zinapoingia kwa kituo ili kujipatia nafasi kupanga abiria,” alisema Ong’era.

“Tunaomba serikali kutuwekea matuta kwa barabara zote ziingiapo hapa kituoni ili wale wako na uzoefu wa kuendesha kwa kasi kutulizwa,” aliongeza Ong’era.

Justine Monari, dereva mwingine naye alisema mara nyingi watu ambao hawana hatia yoyote hugongwa katika kituo hicho kupitia uendeshaji huo wa kasi .

“Tukiwekewa matuta hayo basi huenda visa vya ajali vipungue hapa kituoni,” alisema Monari.