Wafanyibiashara katika soko la Daraja Mbili mjini Kisii wamelalamikia wahudumu wa Matatu ambao huegesha magari yao kandokando mwa soko hilo kwa kusababisha msongamano katika maeneo hayo.
Kulingana na wafanyibiashara hao magari hayakubaliwi kuegeshwa katika soko hilo kwani hakuna steji iliyoko hapo pia waliwalaumu askari wa kaunti ya Kisii ambao walidai hupewa hongo na kuruhusu wahudumu hao kupangia abiria kando kando mwa soko hilo.
Wafanyibiashara hao wakiongozwa na victor Ochoke walilalamikia hali hiyo huku wakiomba shirika la NTSA na askari wa traffiki kuingilia kati kwani msongamano huo husababisha jali katika eneo hilo.
“Kuna askari wa kaunti ambao wanakuwa hapa Daraja Mbili lakini huwa wanaruhusu magari kusimama hapa barabarani zaidi ya saa moja kupanga abiria na hapa si steji,” alisema Victor Ochoke.