Wahudumu wa pikipiki mjini Eldoret waliandamana Jumatatu kufuatia kugongwa na kuuawa kwa mmoja wao kwenye barabara kuu ya Uganda Road. Wakiongozwa na mwenyekiti wao Jeremiah Nyaosa, walisema kwamba waligadhabishwa sana baada ya dereva aliyetekeleza kitendo hicho kuachiliwa na maafisa wa polisi bila kuchukuliwa hatua ya kisheria.
Wahudumu hao walipiga Kambi nje ya offisi ya komishena wa kaunti Hassan Abdi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Nyaosa alilalamika kuwa wahudumu wa bodaboda wamekuwa wakinyanyaswa na kutohakikishiwa usalama na maafisa wa polisi, jambo ambalo limesababisha uadui kati ya vikundo hivyo viwili.
"Maafisa wa polisi wamekuwa kama maadui kwa wahudumu wa pikipiki na tunashuku ya kwamba ndio sababu wamemuachilia dereva aliyemgonga na kumuangaliza moja wetu bila kumchukulia hatua yoyote ya kisheria," Nyaosa alisema.