Wakaazi wa Bamburi wamelalamikia mazingira mabaya yanayosababishwa na upasukaji wa mabombomba ya kupitisha maji taka katika sehemu hiyo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakizungumza siku ya Jumamosi na wanahabari, wakaazi hao walilalamika kwa kusema kuwa hali hiyo inachafua mazingira na kuweka maisha yao hatarini.

Wakaazi hao walisema kuwa wanaishi kwa hofu ya kushuhudiwa kwa mkurupuko wa magonjwa na kuinyoshea kidole cha lawama serekali ya kaunti hiyo kwa kutotimiza wajibu wao.

Wakiongozwa na Pricilar Mandi, wakaazi hao waliilaumu serikali ya kaunti kwa kutochukulia swala hilo kama la muhimu na kukosa kulisuluhisha.

Aidha, wakaazi hao wameitaka serekali ya kaunti na idara husika kutoa muafaka kwa swala hilo ambalo limekuwa kero kwao kwa mda mrefu.

Serikali ya kaunti ilijitetea kwa kusema kuwa wako mbioni kutatua swala hilo, na hali hiyo haitashuhudiwa tena.