Wakaazi wa eneo la Bokole katika eneo bunge ya Changamwe wanakadiria hasara baada ya upepo mzito kung'oa paa za nyumba zao.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mkasa huo ulioshuhudiwa siku ya Jumapili mwendo wa saa tatu asubuhi uliathiri zaidi ya nyumba ishirini.

Mbunge wa eneo hilo Omar Mwinyi alizuru eneo hilo kuwafajiri wakaazi hao na kujadiliana katika kutafuta suluhu mwafaka.

Maafisa wa Shirika la Msalaba Mwekundu pia walifika katika eneo hilo kuwasaidia waathiriwa hao.

Akiongea katika eneo hilo la Bokole, Mwinyi alipendekeza kuundwa kwa shirika litakalokuwa likishughulikia mikasa ya dharura katika eneo bunge hilo.

"Nilipeana shilingi laki moja kwa waathiriwa wa mkasa huo ili kujikimu ki maisha katika muda huu ambao nyumba zao hazina paa,” alisema Mwinyi kupitia mtandao wake wa kijamii.

Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu, hakuna aliyejeruhiwa katika mkasa huo.