Wakaazi wa Nakuru kwenye mtaa duni wa Bondeni wamekashifu kitendo cha mama mmoja kutaka kumuua motto wake mchanga baada ya kujifungua.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Maureen Agiza alidaiwa kujifungua motto wake na kumtupa kwenye choo kwenye mtaa huo.

“Sisi kama wamama tuko na uchungu sana. Mbona mama abebe motto miezi tisa alafu akuje kumtupa hapa? Tuko na uchungu sana,” Edna Moraa alisema.

Agiza alikuwa mwanafunzi katika chuo kimoja mjini Nakuru.

OCS wa kituo cha Bondeni Pascal Mwamba alisema polisi walijulishwa kuhusu kisa hicho na wakazi.

“Tulipigiwa simu na kufika hapo. Polisi walisaidiana na wakazi kutoa motto huyo,” Mwamba alisema.

Akina mama walisema Agiza anafaa kukabiliwa kisheria.

“Ametukasirisha sana, afungwe kabisa,” Mary Nyambura alisema.