Huku msimu wa mvua ukiendelea, waendeshaji bodaboda na magari katika barabara ya Prisons kuelekea Nyamira wamelalamikia daraja la Prisons inayounganisha barabara ya RAM na ile ya Prisons kufuatia mafuriko ya mara kwa mara ambayo yanahofiwa kasababisha maafa.
Mmoja wa madereva wa magari ya kuelekea Nyamira ya kampuni ya Smartline Jason Mukua amesikitikia hali hiyo ambayo alisema kwa wakati mmoja karibu iuwe mwendeshaji Bodaboda mmoja baada ya Mto Nyakumisaro kufurika na kufunika daraja hilo ambapo wanaoendeshaji Bodaboda wengi walibahatisha maisha yao kwa ajili ya kupata pesa kwa wasafiri.
Naye Ben Mogire ambaye ni mhudumu wa mkokoteni aliiomba Serikali ya Kaunti ya Kisii kulikarabati daraja hilo na kuliinua juu kidogo ili kuweza kuepusha maji kufurika na kufunika daraja hilo.
“Inakuwa vigumu na changamoto kubwa kwa wanaoishi ng’ambo ile ya daraja hili kwa sababu hili ndilo barabara la kutumia na maji yakifurika huwa vigumu kwetu kulivukia kwenye daraja hili,” alisema Mogire.
Kwa upande wa biashara, baadhi ya vijana ambao huosha magari karibu na daraja hilo watoa wito kwa wanaohusika na kusema kuwa tangu wiki jana wamepoteza wateja wao ambao wamekuwa wakipitia apo na kuwapa kazi ya kuwaoshea magari.
“Sisi hutegea wateja ambao hutumia barabara hili kuelekea Nyamira au wanaoishi Jogoo Estate. La kusikitisha ni kwamba kwa sasa biashara yetu ya kuosha magari imeenda chini sababu ya mafuriko ya mara kwa mara yanayosababishwa na mvua inayoendelea kunyesha hapa Kisii na kuwapelekea wenye magari kubadili njia zao,” alihoji Sam Bosire mmoja wa wanaoosha magari karibu na daraja hilo.