Baadhi ya wakaazi wa Mawingu katika eneo bunge la Kuresoi kaskazini wametoa wito kwa serikali kumsamehe chifu wao aliyenaswa kwenye kanda video akiwa mlevi na kusimamishwa kazi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wenyeji hao wanasema licha ya kuwa mlevi, naibu wa chifu Joseph Rotich amekuwa akiwahudumia vyema.

“Hata kama alikuwa analewa, chifu Rotich alikuwa mchapa kazi na alikuwa akituhudumia vyema, kumfuta kazi haikuwa hatua nzuri,” Brian Bundotich, mmoja wa wakaazi alisema.

Mkaazi mwingune alidokeza kuwa chifu wao aliitaji ushauri nasaha na wala sio kumfurusha kazini.

Aidha, hatua ya kufutwa kwa chifu huyo, imepokea maoni mseto huku wengi wakisema kuwa hakufaa kufutwa bali kupewa ushahuri na kupelekwa katika kituo cha kurekebishia tabia.

Hata hivyo maoni ya wakenya kwenye mitandao ya kijamii yalionekana kuzaa matunda kwani chifu Rotich alipelekwa katika kituo cha kurekebishia tabia na mwenyekiti wa Nacada John Mututho mji mkuu, Nairobi ili kurekebisha tabia yake ya uraibu wa pombe.

Kulingana na wakaazi hao, Mututho alifanya jambo la busara kwa kumpeleka chifu wao katika kituo cha kurekebisha tabia hatu ambayo walisema itarudisha matumaini yao kuwa attajiriwa tena.