Wakaazi wa Mlolongo wameshauriwa kuhakikisha kuwa mashimo katika eneo hilo yamefunikwa hasa msimu huu wa mvua, kwa vile huenda yakawa hatari yanapojaa maji.
Akizungumza siku ya Jumapili, mwakilishi was wadi ya Mlolongo, katika bunge la Kaunti ya Machakos, Rachael Nduku, alisema kuwa kuna baadhi ya wakaazi waliochimba mashimo na kuyaacha yakiwa wazi.
Nduku alisema kuwa mashimo hayo huenda yakaleta hatari kwa kuwa watoto wanaweza kutumbukia ndani na kuaga dunia.
Aidha, Nduku alisema kuwa amewatahadharisha wakazi hao mara nyingi dhidi ya kutofunika mashimo hayo, lakini wakazi hao hawajatilia maanani ushauri wake, kwa kua bado hawafahau hatari iliyopo.
"Nimekuwa nikiwaomba wenyeji kuhakikisha mashimo yaliyochimbwa yamefunikwa ili kuwaepusha watoto dhidi ya hatari ya kutumbukia ndani,” alisema Nduku.
Aliongeza, "Wakazi wanapaswa kujua hatari iliyopo wanapoyaacha mashimo haya yakiwa wazi hasaa msimu huu wa mvua.