Wakazi katika baadhi ya mitaa mjini Molo wameitaka serikali ya kaunti ya Nakuru kuweka mikakati ya kukabiliana na maji ya mafuriko baada ya mvua kubwa kuendelea kunyesha katika eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa mitaa ya Casino, Green Garden na mtaa wa Tayari mjini Molo, wamesema maji ya mafuriko yanaingia ndani ya nyumba zao pamoja na maduka ya biashara na kusababisha hasara chungu nzima.

Wakizungumza na mwandishi huyu Jumanne, wakaazi hao walisema licha ya serikali kutangaza mwakani 2015 kuwa mvua ya masika itanyesha katika maeneo mbali mbali nchini, serikali ya kaunti ya Nakuru haikuweka mikakati ya kuondoa kero la maji taka.

Naibu mwenyekiti wa wafanyibiashara wilayani Molo bw Morris Okech amesema baadhi ya maeneo wilayani Molo hushuhudia maafaa msimu wa mvua kubwa, huku akiitaka serikali ya kaunti kufungua mitaro ya kuelekeza maji ya mafuriko ili kupunguza hasara.

“Serikali ya kaunti imelala kazini, iamke na kurekebisha mifumo ya maji taka. Serikali kuu pia isaidiani kutengeneza mitaro itakayozuilia kero la mafuriko ya maji ya mvua kila msimu,” alisema Okech.