Wakaazi wa Molo wamekaribisha kukarabatiwa kwa barabara ya Molo-Olenguruone ambao ulianza Jumatatu.
Wakaazi walisema barabara hio imekuwa kero kubwa haswa kwa wakulima katika kusafirisha mazao yao kutoka shambani hadi sokoni haswa nyakati za mvua.
“Hii barabara imekuwa ni kero kubwa hapa,” Joseph Mwangi alisema.
Mwangi, ambaye ni dereva wa matatu kutoka Olenguruone hadi Molo Keepleft, alisema wamekuwa wakipitia hasara sana kutokana na ubovu wa barabara hiyo.
“Magari zimekuwa zikivunja chum asana hapa. Haipiti siku mbili kama hujaenda garage,” aliongeza.
“Kufika sokoni imekuwa shida sana, tunashukuru viongozi waliofanikisha ujenzi huu,” Josphine Nduta alisema.
Wakaazi hao walimshinikiza mbunge wa Molo Jacob Macharia ahakikishe barabara ya Nolo-Kibunja imekarabatiwa