Wakaazi wa Mombasa wameikosoa Shirika la KWS kufuatia visa vya hivi majuzi vya kutoweka kwa simba kutoka mbuga ya kitaifa ya Nairobi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakizungumza na mwandishi huyu siku ya Jumanne, wakaazi hao, wakiongozwa na Abdhala Karim, wamelitaka shirika hilo kudhibiti wanyama hao ambao huwa hatari wanapoingia katika mazingira na binadamu.

Wakaazi hao walisema iwapo hali hiyo itaendelea kushuhudiwa, itawalazimu kuaandamana hadi katika makao makuu ya shirika hilo jijini Mombasa, ili kuonyesha umoja na wenzao wa Nairobi.

“Kwanini watu wawe kwenye hali ya hatari ilihali watu ambao walipokea mafunzo ya kuwalinda wanyama hawa bado wanalipwa na serikali. Tafadhali twaomba serekali iwe macho na kuwachukulia hatua watu ambao wanazembea kazini,” alisema Karim.

Kauli hii inajiri baada ya shirika hilo kutoa tahadhari kufuatia ripoti kwamba simba mwengine ameonekana katika eneo la Hardy mtaani Karen, hali ambayo imezua taharuki kwa wakaazi wa sehemu hiyo.

Shirika hilo lilisema kuwa maafisa wa KWS wametumwa katika eneo hilo kumsaka simba huyo.