Wakaazi wa Mombasa wamelalamikia kuongezeka kwa nauli ya gari maradufu kufuatia mvua ambayo inaeanza kushuhudiwa katika eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongozwa na katibu wa chama cha abiria Abdi Abdilah, wakaazi hao walisema kuwa serikali ya Kaunti ya Mombasa pamoja na Wizara ya Uchukuzi nchini zinafaa kutuma maafisa wake kuangalia hali hiyo, ili wapate afueni.

Akizungumza siku ya Jumapili na wanahabari jijini Mombasa, Abdilah alisema kwamba hali ambayo inashudiwa kwa sasa ya kupandishwa kwa nauli kwa kisingizio cha mvua haifai.

Wakaazi hao wameshinikiza viongozi wa Kaunti ya Mombasa kuingilia kati na kuhakisha kuwa hali hiyo imerekebishwa.