Hatua ya Mahakama ya ICC kutupilia mbali kesi iliyokuwa ikimkabili Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang imezua hisia mseto miongoni mwa Wakenya.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakaazi wa Kaunti ya Mombasa wakiongozwa na Athman Waweru, wamesema kuwa wamefurahishwa na uamuzi wa kesi hiyo kwani jambo hilo litatoa fursa ya serikali kufanya maendeleo kwa wananchi bila vizuizi.

Wakizungumza na mwandishi huyu mjini Mombasa siku ya Alhamisi, wakaazi hao aidha walisema kuwa serikali imetumia kiasi kikubwa cha fedha kwa na kesi hiyo, hivyo ni bora fedha hizo kutumika kwa kuendeleza miradi ya serikali.

"Tunapongeza uamuzi wa mahakama ya ICC na kusema kuwa hatua hii imeleta mwamko mpya Kenya. Fedha zilizotumika ni nyingi na sasa zitasaidia kuwafanyia Wakenya maendeleo,” alisema Waweru.

Hata hivyo, wakaazi hao wameiomba serikali kutowasahau waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi, na kuwafidia licha ya kesi hiyo kutupiliwa mbali.