Zaidi ya watu ishirini wamelazwa katika hospitali toufati katika Kaunti ya Mombasa kutokana na ugonjwa wa homa ya manjano, al maarufu 'yellow fever', ambayo Idara ya Afya katika kaunti hiyo imetoa ilani kuwa huenda ikaathiri watu wengi.
Mkuu wa Idara ya Afya katika serikali ya kaunti ya Mombasa Mohamed Abdi amesema kuwa kutokea mwezi wa Januari, hospitali kadhaa katika kaunti hiyo zimeandikisha ongezeko la watu wanaougua ugonjwa huo.
Abdi amewataka wakaazi kuchukua tahadhari za ki afya, ili kujikinga kutokana na ugonjwa huo.
Mkuu huyo wa idara pia alisema kuwa huenda ugonjwa huo umesambazwa na maji chafu na hali duni ya mabomba za maji zilizoko haswa katika maeneo ya Likoni na Bamburi.
Hata hivyo, Abdi amesema kuwa idara yake imeweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ugonjwa huo hauendelei kusambaa kwa kutibu maji ya matumizi manyumbani na kurekebisha mabomba yote.