Wakaazi Mombasa wametakiwa kutowabagua na kuwatenga waraibui wa dawa za kulevya katika jamii, bali kuwa mstari wa mbele kuwanasua kutoka kwa janga hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Jumanne jijini Mombasa, daktari kutoka kwa afisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) tawi la Mombasa Saade Abdalla, alisema kuwa wengi wa waathiriwa hao wamejihusisha na vitendo vya uhalifu hivyo wanahitaji marekebisho ya tabia zao.

Alisisitiza kuwa hamasisho litawasaidia pakubwa waraibu hao na kuwanasua kutoka kwa utumizi wa dawa hizo.

Kauli hii inajiri baada ya kushuhudiwa kuongezeka kwa idadi ya waraibu wa dawa za kulevya jijini Mombasa.