Wakaazi wa Mshomoroni wanaoabiri gari katika eneo la Buxton wamelalamikia usalama wao kutokana na shimo lililoko katika eneo hilo.
Wakaazi hao walisema kuwa wakisubiri gari wakati wa usiku huwa kwenye hatari ya kuanguka kwenye shimo hilo.
Wakiongozwa na mwenyekiti wa wakaazi katika eneo hilo Kelvin Omondi, wakaazi hao walisema kuwa shimo hilo limekuwa katika eneo hilo kwa muda wa miezi tano sasa.
Omondi alisema kuwa watu wengi katika eneo hilo huanguka na hatimaye kupata majeraha.
Alisema kuwa iwapo hali hiyo ingethibitiwa mapema, basi shida hiyo haingeshuhudiwa katika eneo hilo.
Julius Nyanje, mmoja wa wakaazi wa Mshomoroni alisema kuwa yeye ni mwanafunzi katika Chuo cha Anuai cha Mombasa (Technical University of Mombasa) na mara nyingi hutoka darasani wakati wa usiku.
Aidha, alisema kuwa hali hiyo imesababishwa na ukarabati wa mabomba ya kupitisha maji taka katika eneo hilo.
Nyanje ameiomba serekali ya kaunti na ile ya kitaifa kuangalia swala hilo na kutoa suluhu la haraka kwani huenda shimo hilo likajaa maji msimu huu wa mvua na kuwa tishio zaidi kwa usalama wa watu.
Hata hivyo, aliyepewa kandarasi ya ujenzi wa mabomba ya maji taka katika eneo hilo amesema kuwa shimo hilo liatweza kuzibwa hivi karibuni ili mahali hapo kuwa salama kwa wakaazi.