Mamia ya wakaazi wa Wadi ya Majengo, eneo bunge la Mvita, wamejitokeza kwenye kambi ya matibabu ya bure iliyozinduliwa rasmi na wakfu wa Sheriff Nassir, kwa ushirikiano na serikali ya Kaunti ya Mombasa.
Kulingana na afisa mkuu wa afya katika Kaunti ndogo ya Mvita Anwar Ali, tangu mwezi wa Januari, takribani watu 88 wameathirika na ugonjwa wa homanyongo A ambao unazidi kuenea katika kaunti nzima.
Ali alisema kuwa maradhi hayo husababishwa sana na maji yaliotangamana na virusi vinavyosababisha homa hiyo.
Wakaazi wa eneo bunge la Mvita walitoa shukrani zao kwa mbunge wa Mvita Abdulswamad Nassir, kwa kuandaa kambi hiyo.
Kwa upande wake, mbunge huyo alisema kuwa aliamua kuandaa kambi hiyo ili kuhakikisha wakaazi wa eneo hilo wana afya bora pamoja na kuwakinga dhidi ya maradhi yanayochipuka.