Genge la majambazi ambao idadi yao haijulikani lilivamia kijiji kimoja mjini Naivasha na kuwaiba ng’ombe saba pamoja na mbuzi kadhaa.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Haya yalijiri huku wakazi wa eneo hilo wakitaka kufanyika kwa juhudi za dharura ili kuweza kudhibiti wizi huo ambao umeendelea kukidhiri.

Kwenye tukio hilo la usiku wa kuamkia Jumatano, wezi hao walivamia kijiji cha Mirera na kuiba mifugo hao katika boma moja.

Mkazi mmoja Jackson Nguro alisema kuwa wezi hao walivunja zizi la mifugo hao na kuwaondoa bila ya kujulikana licha ya kituo cha maafisa wa kupambana na wizi wa mifugo kuwa kilomita chache kutoka eneo hilo.

"Tunashangaa jinsi ngombe hao walivyoibwa kwa sababu licha ya kuwa na kambi ya ASTU hapa karibu hakuna aliyesikia wala kujua," alisema Nguro. 

Afisaa mmoja wa polisi wa ngazi ya juu ambaye hakutaka jina lake litajwe amedhibitisha tukio hilo na kusema kuwa tayari wameweza kuwapata Ng’ombe watatu kati ya saba walioibiwa na kuwataka wakazi hao kuwa na subra huku wakiendelea kuwatafuta wale wengine.