Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Afisaa wa afya wa kaunti ya Nakuru Samuel King’ori amewataka wakaazi kuchoma miili ya wapendwa wao waliofariki kutokana na uhaba wa nafasi katika makaburi ya umma.

Akizungumza Jumatatu alisema makaburi Nakuru yamejaa.

Alisema notisi ilitolewa kutoka kwa afisi yake kwa mujibu wa sheria ya afya ya umma inayomruhusu kufunga makaburi yote yaliyojaa, huku sheria hiyo ikimpa mamlaka ya kutoza yeyote faini ya shilingi 1,500 anayeendelea kuzikana katika makaburi hayo yaliyo jaa.

Ingawa serikali ya kaunti ya Nakuru inaendelea kujibidiisha kutafuta ardhi iliyo na mchanga unaohitajika kisheria kutengewa kwa ajili ya makaburi, hadi kufikia sasa jitihada hizo hazijafua dafu.

Ijapokuwa kaunti ya Nakuru ina mchanganyiko wa watu kutoka tabaka na tamaduni mbalimbali, huenda ikawa kizuizi kikubwa kuwashawishi ili waweze kuchoma miili ya wapendwa wao waliyofariki.