Aliyekuwa mwekahazina wa chama cha Kanu nchini Dkt William Nyakiba amejitokeza kuwasihi wananchi kuwapigia kura viongozi wa nyadhifa za kisiasa kutokana na utendakazi wao.
Akiwahutubia wanahabari mjini Nyamira siku ya Jumapili Nyakiba alisema kuwa yastahili wananchi wawapigie kura viongozi kulingana na utendakazi wao.
“Ni ombi langu kwa wananchi kuhakikisha kuwa wanawachagua viongozi wa nyadhifa za kisiasa kwa kuzingatia utendakazi wao na wala sio kwa kuzingatia milengo ya kisiasa wanayoiegemea," alisema Nyakiba.
Nyakiba aidha alichukua fursa hiyo kutangaza azma yake ya kuwania kiti cha ugavana kwenye kaunti ya Nyamira huku akiwataka wakazi kumpigia kura.
“Uchaguzi uliopita niliwania kiti cha ugavana lakini sikufanikiwa kushinda. Ni ombi langu kwenu kwamba tutapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ujao, munipigie kura kwa wingi ili tuweze kubadilisha hali ya uongozi huku Nyamira," aliongezea Nyakiba.