Wakaazi katika ukanda wa Pwani wamehimizwa kudumisha amani, uiano na kutobaguana kwa misingi ya kidini, kikabila wala kisiasi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kiongozi wa Dini ya Kiislamu katika Kaunti ya Kwale Sheikh Kassim Zani, amesema kuwa kuna umuhimu wa kuishi kama ndugu bila ya kuangaliana rangi, dini, vyama vya kisiasa wala ukabila.

Akizungumza katika kongamano la viongozi wa kidini lililoandaliwa katika hoteli moja mjini Mombasa siku ya Ijumaa, Sheikh Zani aliwahimiza wakaazi kudumisha amani.

Sheikh Zani alisema kuwa uiano ni muhimu katika jamii kwa kuwa ndio unaoleta amani na utangamano.

Alisisitiza umuhimu wa kuishi kama ndugu bila ya kuangalia rangi wala dini mtu anayotoka, kwa kusema kuwa ubaguzi huenda ukaleta uhasama wa kijamii na kuvurugu usalama wa eneo la Pwani kwa jumla.

“Tunawaomba wakaazi wa eneo la Pwani kuhakikisha kuwa mnawapenda jirani zenu na kuisha kama ndugu bila ya kujali kabila, dini wala chama cha kisiasa, ili kuhakuikisha kuwa jamii inatangamana na kuishi kwa Amani,” alisema Sheikh Zani.

Kuhusiana na suala la uamuzi wa Mahakama ya ICC dhidi ya kesi iliokuwa ikiwakabili Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang, Sheikh Zani aliwaomba Wakenya kuukubali uamuzi huo na kuongeza kuwa walioathirika watalipwa fidia kufuatia ahadi serikali imeweka kwa Wakenya.