Mwanasiasa Ananiah Mwaboza katika hafla ya awali. Amewataka wakaazi kuwa imara tunapokaribia uchaguzi mkuu ili kuepuka kulaghaiwa na viongozi wabinafsi. Picha/ the-star.co.ke

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi wa Kaunti ya Mombasa na ukanda wa Pwani kwa jumla wamehimizwa kujitenga na wanasiasa wanaowadanganya kwa kuwapa pesa, hasa wakati huu ambapo kampeni zinazidi kupamba moto.Mwanasiasa kutoka Mombasa, Ananiah Mwaboza, awewataka wakaazi kuwa imara tunapokaribia uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti, ili kuepuka kulaghaiwa na viongozi wabinafsi.Akizungumza kwenye kikao na wanahabari mjini Mombasa, Mwaboza alisema kuwa ili kuwe na maendeleo katika Kaunti ya Mombasa, sharti wakaazi wawachague viongozi bora.Mwaboza amewahimiza wananchi kuwateua viongozi kulingana na sera zao za maendeleo bali sio kwa kukuzingatia dini wala kabila.Wakati huo huo, mwanasiasa huyo ameikosoa serikali ya Kaunti ya Mombasa kwa madai ya kushindwa kutekeleza matakwa ya wananchi.“Serikali ya kaunti inajihusisha katika ufujaji wa raslimali ya umma jambo linalochangia maisha duni miongoni mwa wakaazi wa Mombasa,” alisema Mwaboza.