Wakaazi wa kijiji cha Sasimwa katika kaunti ya Nakuru wanalazimika kulala na mifugo wao kwenye chumba cha kulala kutokana na wizi ambao unaendelea katika kitongoji hicho.
Hii ni kutokana na ongezeko la wizi katika eneo hilo.
John kamau, mkaazi wa Sasimwa na ambaye hufuga mgombe na mbuzi, alisema ana uchungu mwingi baada ya ngombe wake wa maziwa kuibiwa.
Kamau alisema walijaribu kutafuta ng'ombe hao lakini hawakufanikiwa kukata.
Kamau anasema ingawa walimpata ngombe mmoja katika kijiji jirani cha Sirikwa akiwa amefungwa msituni, hawajaweza kujua ni kina nani ambao wanahusika na wizi huo.
David Ngare naye alisema kuwa mbuzi wake waliibiwa Jumatatu usiku na bado hawajawapata.