Transparency International-Kenya, Ijumaa lilizindua rasmi zoezi la kukusanya sahihi Kondele jijini Kisumu katika msukumo wa kupinga hatua ya wawakilishi wadi kupokea marupurupu yanayozidi shilingi elfu 124, 800 kila mwezi.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni chini ya kauli mbiu #RudishaMaliYangu.

Zoezi hili linaongozwa na mwakilishi wa shirika hilo tawi la Kisumu wakili Benjamin Maina kwa ushirikiano na Dennis Indiri.

Maina amesema wakaazi wengi Kisumu wamechangamkia zoezi hilo huku wengi wakifika katika eneo la Kondele kushiriki kutia saini zao katika ombi la kutathmini ili kurudisha marupurupu yasiokuwa halali. (Audit and recover illegal sitting allowances).

Hata hivyo, baadhi ya wakaazi wameonekana kukataa kutia sahihi zao kutokana na kile wanachosema huenda zoezi hilo ni njama tu ya kuchukua nambari zao za kitambulisho kwa lengo la kuzishirikisha katika zoezi la kupiga kura mwaka ujao.

Monica Achieng, mmoja wa wakaazi hao, aliteta vikali kuhusu swala la kuitisha wananchi wanaotia sahihi zao nambari za kitambulisho na licha ya changamoto hii wawakilishi wa shirika la Trasnparency International walifanikiwa kuwashawishi wananchi kuhusu umuhimu wa zoezi hilo.