Wakazi wa Jimbo la Uasin Gishu wana kila sababu ya kutabasamu baada ya serikali ya Jimbo hilo kuzindua miradi mahususi inayolenga kukabili uhaba wa maji katika Jimbo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakazi wa jimbo la Uasin Gishu wana kila sababu ya kutabasamu kwani kwa miezi michache zijazo hawatakua na matatizo ya uhaba wa maji ambao umekua donda ndungu kwa miezi kadhaa hasa kwa mitaa kama vile langas na hata huruma.

Katika mahojiano na ripota huyu, Waziri wa Mazingira maji na Mali Asili katika Jimbo hilo Mary Njogu alisema kwamba idara hiyo imezindua mradi wa maji wa Elgarini ambao unanuia kuhakikisha usambazaji wa maji ya kutosha katika mitaa ya Munyaka, Kapsoya na Kimumu hapa mjini Eldoret.

Aidha Njogu ameongeza kwamba wamezindua mradi mwingine katika eneo la Uwanja Ndege utakaowahakikishia wakazi wa Mtaa wa Langas, Racecourse na mitaa mingine yalioko karibu usambazaji wa maji safi.

Kando na miradi hiyo, idara hiyo pia ina miradi mingine inayojumuisha bwawa la Cheboin eneo la Kipkabus na mradi nyingine katika eneo la Leseru ambapo serikali la Jimbo linashirikiana na wafadhili kutoka Italia.

Waziri huyo pia ameongeza kwamba katika mwaka ujao wa kifedha wana mpango wa kuyakarabati mabwawa na pia kuchimba visima angalau viwili katika kila Jimbo ndogo ili kuwawezesha wakaazi kupata maji safi kwa matumizi yao ya kila siku na pia ya kunyunyizia mimea yao.