Share news tips with us here at Hivisasa

Wakaazi wa wadi ya Birongo eneo bunge la Nyaribari Chache,  Kaunti ya Kisii wamewaomba maafisa wa usalama katika eneo hilo kuweka usalama katika eneo hilo kutokana na wakora wanaowasumbua wakaazi hao haswa wakati wa usiku.

Wakiongea siku ya Alhamisi katika sehemu ya Keumbu wakati Gavana wa kaunti ya Kisii, James Ongwae alipotembea sehemu hiyo kukagua baadhi ya miradi ya maendelea katika sehemu hiyo, wakaazi hao walisema kuwa hali ya usalama katika sehemu ya Birongo imedorora na kumwomba gavana aingilie kati ili kuwasaidia na kuleta suluhu mwafaka ya usalama.

“Hatulali usiku kwani kuna watu wamejitokeza kufanya uhalifu katika wadi yetu na tunaomba idara husika kushughulika jambo hili kwa haraka ili kuleta suluhu katika eneo hili," alisema Simeon Gichana, mkaazi.

Aidha, walimwomba gavana Ongwae kuwasaidia ili usalama uweze kuimarika katika eneo hilo ili waweze kujiendeleza kimaisha na kuinua viwango vya uchumi katika kaunti ya Kisii.

“Tunakuomba gavana wetu utusaidie ili usalama uweze kuwa katika wadi yetu kwani tunaishi na uoga. Tunasambuliwa hata wakati tunatoka kazini masaa ya jioni jambo ambalo limeleta shida kubwa miongoni mwa wafanyi biashara,” alisema Elijah Onyoni, mkaazi.

Kwa upande wake, gavana James Ongwae alisema kuwa atahakikisha kuwa wamekuwa na mkutano na wasimamizi husika wa idara ya usalama ikiwemo kaunti kamishena wa kaunti ya Kisii Chege Mwangi na naibu wake Philip Soi ili kutatua shida hiyo.

“Nitahakikisha kuwa tumekuwa na mkutano wa usalama katika eneo hilo hivi karibuni ili tuweze kujua shida iko wapi ili kuleta suluhu la mapema,”alisema Ongwae.