Wakaazi wa Engobor, Kapkures Nakuru wana kila sababu ya kutabasamu baada ya tatizo la maji kushughulikiwa kupitia mchango wa harambee.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Uhaba wa maji eneo hilo katika siku za hivi karibuni ulilazimu wakaazi kutembea masafa marefu wakitafuta bidhaa hiyo. Kisima cha Engobor kitaimarishwa katika kutoa huduma hiyo.

Akizungumza na wanahabari Alhamisi baada ya hafla hiyo ya harambee, David Karuri anayenuia kuwania ubunge Nakuru Magharibi alisema kuwa maji safi ni haki ya kila mmoja na haifai kukosekana.

"Ni jambo la kusikitisha kwamba wakaazi wa Engobor wanakosa maji safi ilhali ni haki yao kama walipa ushuru,"alisema Karuri.

Hata hivyo alisema kuwa swala hilo litashughulikiwa kwa ushirikiano na mwakilishi wadi hiyo Joseph Lang'at.

Karuri aliongeza kuwa kama njia mojawapo ya kuhakikisha uongozi bora ni kuwashirikisha wananchi katika miradi maalumu.