Wakaazi wa Gesima katika eneo bunge la kitutu Masaba wameombwa kuchagua kwa makini kiongozi yeyeyote anayetaka wadhifa wowote katika eno hilo ili kupata maendeleo.
Akiongea siku ya Jumapili katika hafla ya mchango wa kanisa ya Matutu PAG iliyoko katika wadi ya Gesima, kaunti ya Nyamira, Mokaya Makori, ambaye ana azma ya kuwania kiti cha mwakilishi katika wadi hiyo alitangaza kuwa amejibwaga uwanjani kwa kinyanganyiro cha mwaka wa 2017, ambapo amewaomba wakazi hao kumwangalia kama hataweza.
“Nawahakikishia kuwa nimejibwaga uwanjani kwa kinyanga’nyiro cha kuwawakilishi katika bunge letu la kaunti la Nyamira ifikapo mwaka wa 2017, kwa hivyo ni wajibu wenu kunipiga msasa hadi wakati huo kama mtaona nitaweza mtanipigia kura,” alisema Maroko.
Aidha, aliwaomba wakristo kuwa katika msitari wa mbele kuhubiri amani kwa watu wote na kuombea viongozi wote wa nchi ya Kenya ili waweze kuendelea kuinua viwango vya uchumi na biashara.
Mokaya aliwaomba vijana wote katika wadi ya Gesima kutumia wakati wao wa likizo kwa njia ya kujiendeleza na kijiepusha na mambo yatakayo waletea madhara kwao.
Baadhi ya waliohudhuria halfla hiyo waliwaomba viongozi wote wa Nyamira kungana pamoja bila kujali chama na ukoo wanamotoka na kufanya kazi kwa pamoja ili kuinua viwango vya maendeleo katika kaunti hiyo.
“Tunaomba viongozi wote walioko mamlakani kwa sasa kufanya kazi kwa pamoja bila kujali chama na ukoo wanakotoka kwa kuwa hicho ndicho kitu kinachotusumbua kama sisi watu wa nayamira,” alisema Grace Nyanchama.
Katika hafla hiyo walichanga zaidi ya shillingi elfu mia moja, huko Maroko akitoa mchango wake wa shillingi elfu ishirini huku akiwahidi kuwatumia elfu mia moja.