Wakaazi wa wadi ya Gesima, iliyoko katika eneo bunge la kitutu Masaba, kaunti ya Nyamira, wamewaomba  viongozi wote wa kaunti hiyo kushirikiana ili kuleta  maendeleo bila kujali ukoo na chama kilichowachukua uongozini.

Share news tips with us here at Hivisasa

Aidha, wamewaomba viongozi hao kuchukulia swala la maji kuwa la muhimu, na kuchimba visima katika maeneo mbali mbali ili kuepuka changamoto sinazowakumba kutokana na ukosefu wa maji hasa wakati wa kiangazi.

Wakiongea  siku ya Jumatatu katika chemichemi ya matunwa wakati walijitolea kuondoa uchafu katika chemichemi hiyo, wakaazi hao wameiomba serikali ya kaunti ya Nyamira kutenga pesa zitakazotumika kuchimba visima katika kaunti hiyo ili siku sijazo wasikumbane na shida ya maji wakati wa  kiangazi kama msimu ule walioshuhudia kiangazi kwa miezi minne.

“Tunaomba serikali ya kaunti kuchimba visima ambavyo vitatusaidia siku sijazo kwa kuwa wakati tulishuhudia kiangazi tulisumbuka sana, kama tungekuwa na  visima hivyo, hatungekuwa na shida wakati wa kiangazi,” alihoji Samwuel Kenani, mkaazi.

 Aidha, wamemwomba mwakilishi wa wadi hiyo Kennedy Nyameino kushughulikia jambo hilo na kufikisha mswaada katika bunge la kaunti hiyo ili pesa kutengwa sitakazotumika kuchimba visima, kwani  mvua siku hizi hunyesha kwa mda mfupi.

Pia wamemwomba mwakilishi huyo kupea sekta ya maji na barabara nafasi ya kwanza na kukarabati baadhi ya chemichemi zilizoanzishwa na waliotangulia uongozini kama ile ya Matunwa, Riobiri, miongoni mwa nyinginezo .

“Kuna baadhi ya chemichemi zilizoanzishwa na viongozi waliong’atuka mamlakani, kwa hivyo tunamuomba Nyameino aendeleze miradi  hiyo ili maendeleo yaweze kunawili katika wadi yetu na kaunti nzima ya Nyamira,” alielezea Peterson Kebaso.