Wakaazi kutoka Kaunti ya Kisii na ya Nyamira wanaendelea kutuma risala zao za rambirambi kwa familia ambazo ziliwapoteza wanao katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa katika Chuo Kikuu cha Garissa mapema mwezi huu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi hao sasa wameiomba Serikali ya Kaunti hizo Mbili kuwatafutia manusura Chuo mbadala watakapoendelea na masomo yoa kwa kuwa hawataki wanao kurudi tena katika sehemu hizo ‘hatari’.

Wakiongea hiyo siku ya Jumatatu, Baadhi ya wakaazi woliofika katika uwanja wa Gusii kwa hafla ya maombi ya kuwaaga wenzao waliouwawa kwenye shambulizi la Garissa walielezea kuwa wamekosa imani na sehemu hiyo na kusema kamwe hawatawaruhusu wanao kurudi Kaskazini Masharika kabla ya usalama wa kutosha uwekwe na Serikali.

“Masomo ni nguzo ya kesho katika jamii, lakini kwa bahati mbaya watoto upoteza maisha yao bila hatia yoyote wanapoenda kutafuta masomo yao katika sehemu zingine za Kenya, kitu ambacho kimetukera sana na kutufanya tukose imani na sehemu hizo,” alisema Mokaya Joshua mkaazi wa eneo hilo.

Aidha, wakaazi hao wameiomba Serikali ya Kaunti ya Kisii na ile ya Nyamira ikiongozwa na Gavana wa Kisii James Ongwae, na mwenzake wa Nyamira Gavana John Nyagarama kushirikiana na viongozi wengnei ili kutafuta Vyuo vingine vilioko sehemu pana usalama kwa walionusurika kifo ili wanafunzi hao wapate nafasi ya kuendelea na masomo yao.

“Tunaomba Serikali ya Kaunti ya Kisii na Nyamira kuwashughulikia wanafunzi walionusurika Chuo watakapojiunga ili waendelee na masomo yao,” alisema Grace Onchoke mkaazi wa Eneo hilo.

Kulingana na waakazi hao na viongozi waliodhuria hafla hiyo ya maombi iliyofanyika siku ya Jumatatu, mashambulizi ya kigaidi  ambayo yametekelezwa nchini Kenya, jamii ya Abagusii imewapoteza watu wengi hasa kwenye shambulizi lililotekelezwa  katika maeneo ya Mandera ambalo liliacha zaidi ya walimu saba wakiuwawa na lile la Garissa zaidi ya watu 10 kuuwawa kitu ambacho kimewaacha wengi kwa mshangao mkubwa.