Ujenzi wa vituo vya kutekea maji katika maeneo ya Jacaranda Wanyororo B umewapa msisimko wa aina yake wenyeji, baada ya kukaa kwa miaka 30 bila ya maji safi ya matumizi.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakizungumza na mwandishi huyu Jumanne, wakaazi hao walisema: Wanaosema ugatuzi haufanyi kazi, ni maadui wa maendeleo.”

Walisema hayo wakati mwakilishi wa wadi ya Bahati Peter Nderitu Mwangi alipokua akikagua kazi ya ujenzi wa mradi huo.

“Sasa si wakati wa ahadi hewa, tunataka watu ambao wanafanyakazi. Kupata maji ya mifereji baada ya miaka 30 ni kama miujiza,” alisema John Mwangi.

“Naye Joyce Wanjiku alisema : “Tulikuwa tunaenda kununua maji lita 20 kwa shilingi kumi, kilomita tano kutoka nyumbani. Hii ni afueni kwetu”

“Sasa hata mabwana hawatatupotea tena kwa sababu tunakuwa wachafu, akasimulia binti kwa jina Mary Kamau.

Mwakilishi wa wadi Nderitu alisema ananuia kuhakikisha wadi hiyo yote imepata maji ya mifereji kabla ya uchaguzi mkuu ujao.