Wakaazi wa Mwache, Wadi ya Kasemeni, katika mpaka wa Kaunti ya Mombasa na Kwale wamesema wanahofia mmomonyoko mkubwa wa udongo ambao huenda ukashuhudiwa pindi mvua zitakapoanza.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakiongozwa na Thomas Kamanza, wakaazi hao walitoa ombi kwa vyombo vya habari na mashirika ya kijamii kutoa hamasisho kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuzuia mmomonyoko huo kwa kupanda miti kwa wingi.

Sehemu ya Mwache ni sehemu ambayo hushuhudia sana mmonyoko wa udongo kutokana na mifugo mingi ambao hutafuta lishe katika eneo hilo, na hivyo kuliacha eneo hilo kusalia bila nyasi.

Wakaazi hao walilalamika kwa kusema kuwa huwa hawaoni msaada wowote kutoka kwa serekali wala mashirika.

Aidha, walisema kuwa hali hiyo huwa kero kwao ikizingatiwa kwamba hao ni jamii ambayo hutegemea sana ufugaji.

Msimu wa mvua za masika mifugo wengi huangamia na watu wengi kuachwa bila makao.

Itakumbukwa kuwa hali hiyo pia hushudiwa katika maeneo ya Rabai na Mwakirunge kwenye Kaunti ya Mombasa.