Wakaazi wa wadi ya Nyota wanateta ongezeko la wizi wa mifugo kwenye eneo hilo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wakaazi hao wanasema kuwa wezi wa mifugo wanazidi kuwahangaisha na wanalazimika kulala macho usiku kucha kulinda mifugo wao. “Hapa hatulali kutokana na wizi huo. Tunawaomba polisi wahakikishe kuwa tunapata usalama wa kutosha,” Hillary Ng’eno alisema.

Hayo yanajiri wakati ambapo mshukiwa mmoja wa wizi wa mifugo alivamiwa na kuchomwa na umatiwa watu kwenye eneo la Keringet kwenye wadi hiyo.

MCA wa wadi hiyo Njuguna Gicamu alisema swala hilo ni la kusikitisha na kuwataka wananchi wasichukue hatua mikononi mwao.

Vile vile aliwataka polisi kuhakikisha kuwa wanawapa wakazi suluhu.