Wakaazi wa Kiamabundu, eneo bunge la Nyaribari Chache, kaunti ya Kisii, wamemuomba chifu na naibu wake George Nyamwaka kufanya uchunguzi ili kubaini wezi ambao wanawasumbua wakazi hao.
Wakiongea na mwadishi huyu jana katika maeneo ya Kenonga, wakaazi hao walisema kuwa wameghadhabishwa na kuchozwa na vitendo vya wezi na kusema kuwa wezi hoa wamewarudisha nyuma Kiamaendeleo.
“Kila siku tunakuwa na uoga wa kufanya maendeleo kwa kuwa wezi hao wanasuburi tuwafanyie kazi jambo ambalo limekuwa la ajabu kwetu kama wakaazi,”alisema Mokaya James, mkaazi.
Wakaazi hao wamesema kuwa wamechoshwa na vitendo hivyo na kuwaomba chifu na manaibu wake kufanya uchunguzi ili wezi hao waweze kutiwa mbaroni na kuchukuliwa hatua kali ya kisheria.
“Tunaomba chifu na naibu wa chifu kufanya uchunguzi ili wezi hao waweze kuchukuliwa hatua kali ya kesheria kwa kuwa wamekuwa na mazoea ya kupora watu,”alisema Velida Moraa, mkaazi
Aidha wamewaomba machifu hao kuwachukulia hatua kali wazazi ambao wanao hawaendi shule kwa kuwa wanahofia kuwa watoto hao huenda ndio huiba au ndio wanaowaunganisha wezi katika maeneo hayo.
Haya yote yanajiri baada ya wezi hao kuiba ng’ombe na mtungi wa maji kutoka kwa boma moja wiki mbili tu baada ya kuiba pikipiki mbili kutoka kwa boma hilo.
Wakaazi hao wamewaonya wezi hao na kusema siku zao zimehesabiwa.