Wakaazi wa mtaa wa Kidogo Basi wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kupewa hati miliki na serikali ya kaunti.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Jumatano katika eneo hilo la Kidogo Basi katika hafla ya kuwakabidhi wakaazi hao hati miliki, Gavana wa Kaunti ya Mombasa Hassan Joho alisema kuwa wakaazi hao sasa wana haki ya kumiliki ardhi hiyo.

“Baada ya kuishi kama maskwota kwa muda wa miaka ishirini, wakaazi wa Kidogo Basi sasa ni wamiliki halali wa ardhi,” alisema Gavana Joho.

Gavana Joho alisema kuwa hatua hiyo imefanikishwa na juhudi za serikali ya Kaunti ya Mombasa kwa ushirikiano shirika la Kidogo Basi.

Joho aliwahakikishia wakaazi wa Mombasa kuwa serikali ya kaunti inafanya kila juhudi kuhakikisha kuwa suala la migogoro ya ardhi katika kaunti hiyo linapata suluhu la kudumu.