Wakaazi wa mji Kisii na viunga vyake wameombwa kupiga ripoti kila mara kwa wasimamizi wa maji na usafi, wakati mifereji ya maji na majitaka inapovuja katika mahali wanamoishi ili kushughulikiwa kwa haraka.
Akiongea na mwandishi huyo, msimamizi husika wa majitaka katika Kaunti ya Kisii Evans Simba aliwaomba wakazi wote kuripoti wakati shida ya maji au majitaka.
“Wakazi wote wanastahili kupiga ripoti kwa haraka ili nasi tuweze kufika mahali hapo kwa haraka na kuwasaidia kwa kuwa hiyo ni kazi yetu,” alisema Simba
Aidha, Simba aliongezea kuwa yeye na maafisa wote wa shirika hilo wako tayari kila wakati kushughulikia na kurekebisha mifereji hiyo ili kuhakikisha kuwa mahali watu wanamoishi ni pasafi.
Kulingana na wakazi wa Kisii, mifereji ya majitaka mingi huvuja, hasa wakati huu wa mvua nyingi inayoendelea kunyesha na kutoa uchafu kwa mifereji, uchafu unaohatarisha afya ya wakazi hao.
Kwa sasa wamewaomba wasimamizi wa GWASCO kurekebisha mifereji, na hasa kuwaomba kubadilisha mabomba kwa kuwa yaliyotumika hapo mbeleni yalikuwa gushi na nyembamba, jambo linolosababisha kuvuja kwa mifereji hiyo kila mara,
“Tunaomba wazimamizi hao kurekebisha na kubadilisha mabomba hayo kwa kuwa kila siku yanavuja,” alisema Frolence Okongo, mkaazi.
Kwingineko wameomba wanaojenga nyumba katika mji wa Kisii na Viunga vyake kutoelekeza mirereji ya majitaka kuelekea mtoni, kwa kuwa wengi wa wakazi hutumia maji hayo kwa kuoshea nguo na hata wengine hutumia kuoshea Mboga, jambo litaweza sababisha magonjwa ya maji.