Baadhi ya wakaazi wa mji wa Kisii wameupongeza uongozi wa jimbo la Kisii kwa kukarabati barabara ambazo zimekua kero kwa wengi kwa mda mrefu.
Hii ni baada ya barabara inayounganisha barabara ya kuelekea Nyamira na ile inayoelekea Migori kufanyiwa ukarabati.
Kulingana na mkaazi wa eneo hilo Philip Moseti, ugatuzi wa rasilimali umekua nguzo muhimu katika maendeleo kwa jimbo la Kisii.
“Kwa sasa, nafurahia matunda ya ugatuzi, barabara mbazo zimekua dondandugu kwa mda sasa zimelainika na usafiri hauna tatizo,” alisema Moseti.
Halikadhalika, barabara inayoelekea Bosongo pia haijaachwa nyuma, kwani imefanyiwa ukarabati na wakaazi wana kila sababu ya kufurahia.
Kulingana na mfanyibiashara Bi. Moraa, amenufaika pakubwa kutokana na ukarabati wa bararbara.
Anasema yeye hutegemea barabara anaposaifirisha mboga zake akizipeleka mjini kwa uchuuzi.
“Hapo zamani nilikuwa napata changamoto ya usafiri kwasababu ya barabara mbovu japo siku hizi nimepata afueni baada ya barabara kukarabatiwa” alisema Moraa.
Waziri wa usafiri kwenye jimbo la Kisii Zablon Ongori ameelezea kuwa uongozi wa Gavana Chris Ongwaye una mipango mahususi ya kuwafaidi wakaazi ili kuleta maendelea kwenye jimbo hilo.
“Lengo letu kama uongozi wa kaunti hii ni kuhakikisha wakaazi wamenufaika na ugatuzi kikamilifu jinsi inavyoeleza sharia ya ugatuzi,” alisema Ongori.
Huku wakaazi wa jimbo la Kisii wakiendelea kufurahia mazuri ya ugatuzi pia wenye magari wana kila sababu ya kufurahia kwani vyegezo vya magari na vimekarabatiwa mjini Kisii na njia za wanaotembea.