Wakaazi katika mji wa kisii wameombwa kujua hali yao ya kiafya kwa kutembelea vituo vya kiafya vya serikali ambavyo hutoa huduma hii bila ya malipo yoyote.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea afisini mwake waziri wa afya kwenye kaunti ya kisii, Mary Angima, amesema kuwa ni jambo la busara kwa kila mkaazi kujua hali yake ili kujua namna ya kupanga maisha yake.

“Kujua hali zetu ni jambo la muhimu na ninawaomba wakaazi kutembelea vituo vya kiafya vya serikali ambapo watapata huduma hii bila malipo,” alisema Angima.

Halikadhalika ameongezea kuwa wakaazi wengi husahau halizao na hivyo kuwa hatarini ya kuambukizwa au kuambukiza virusi hatari vya ukimwi.

“Ni jambo la kushangaza kuwa wakaazi wengi kwa kutokujua hali zao huambukizwa au kuambikiza virusi vya ukimwi na jambo hili huathiri sana jamii,” aliongezea Angima.

Alisikitika kuwa vijana ambao ndio viongozi wa kesho ndio waliyo kwenye hatari kubwa.

Alisema kua hali hii huenda ikaiacha jamii bila ya watu wanaoweza kuisaidia kiuchumi na maendeleo.

“Vijana ndio ambao ni viongozi wa kesho lakini kulingana na uchunguzi wa kiafya wamo kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya ukimwi,” alisema Angima.

Vilevile amepongeza wadau wengine kwa kusaidia wakaazi kujua hali zao kwa mfano taasisi za elimu kama vile chuo kikuu cha kisii na mashirika ya kibinafsi.

 “Naziunga mkono taasisi za shule na mashirika yasiyokua ya kiserikali kwa kuwa katika msitari wa mbele kuhamasisha umma kuhusu suala la hali zao,” alisema Angima.