Wakaazi katika mji wa kisii wamehimizwa kupanda miti kwa wingi kama njia moja ya kulinda na kuhifadhi mazingira.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza afisini mwake waziri wa mazingira na mali asili Skitter Wangesi Mbugua,  amewataka wakaazi kupanda miti ili kulinda mazingira.

“Ninawaomba wakaazi kupanda miti kwa wingi kama njia moja ya kulinda mazingira,” alisema Mbugua.

Aliongezea kuwa kupanda miti kuna manufaa mengi kwa mfano kuzuia mmonyoko wa udongo hasa maeneo yenye miinuko, hewa safi na kuongezeka kwa kiwango cha mvua.

Halikadhalika amesema kuwa serikali ya kaunti ya kisii ina mipango mahususi ya kulinda na kuhifadhi mazingira kwa vizazi vya sasa na vya usoni.

Vilevile amewaonya wale wanaokata miti kiholela bila kupanda mingine watachukuliwa hatua kali za kisheria.

“Nawaonya wale wanaokata miti kiholela watachukuliwa hatua za kisheria wakipatikana,” alionya Mbugua.

Amewataka wakaazi kushirikiana na wadau wote katika jitihada kabambe za kulinda mazingira.

”Suala la kulinda na kuhifadhi mazingira ni ushirikiano kati ya wakaazi na wadau wote na heko kwa wale wanaopanda miti,” alisema Mbugua.