Wakaazi wa Wadi ya Kisii ya Kati eneo Bunge la Nyaribari Chache wameipongeza Serikali Kuu kwa kuwapokeza pesa za kuinua jamii.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakiongea siku ya Jumatano katika  sehemu ya Gekomu, wakaazi hao waliipongeza Serikali Kuu kwa mradi huo wa Inua Jamii ambao unawasaidia mayatima na wakongwe ili kujiendeleza kimaisha.

“Ninaipongeza Serikali Kuu kwa kutukumbuka kwa kutupokeza pesa hizo ambozo kwa sasa zimenisaaidia pakubwa kulipa karo kwa mayatima ambao nasimamia,” alihoji Danniel Mogeni anayesimamia mayatima.

Aidha Mogeni ameiomba Serikali Kuu kuongeza kiwango hicho cha pesa kwa kuwa kuna mahitaji mengi ambayo yanahitajika kwa mayatima kushughulikiwa.

“Mayatima huwa wanahitaji mambo mengi kwa hivyo naomba Serikali Kuu kuongeza pesa hizo ili mahitaji yao yaweze kuyafikiwa ili wajiendeleze kimaishha,” aliongezea Mogeni.

Hapo awali wakongwe na mayatima walikuwa wamelalama kutokana na kufeli kwa mashine ya Benki ya KCB lakini kwa sasa wanaipongeza kwa kuwa imewapokeza pesa hizo ambazo zilianza kupeanwa tena siku ya Jumamosi katika maeneo mbali mabali kinyume na tarehe 29 mwezi huu walioambiwa.

Kwingineko wasimamizi wa Inua Jamii wamewaomba wanaosimamia wakongwe na mayatima kuwa na uwazi wakati wanapozipata pesa hizo bila kuwanyima wakongwe na mayatima pesa zao.

Kulingana na wasimamizi hao, watu wengi hutumia pesa hizo kujifaidi wao wenyewe bila kujali masilahi ya mayatima na wakongwe jambo ambalo ni kinyume na sheria za pesa hizo.