Wakaazi wa kaunti ya Kisii wameombwa kuchemsha maji kabla ya kunywa ili kuepukana  na magonjwa yanayosababishwa na maji chafu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akiongea na mwaandishi huyu siku ya Jumamosi katika hospitali ya  Rufaa na mafunzo ya Kisii, mhudumu wa Afya ya Jamii Kepha King’oina aliwaomba waakazi wote kuchemsha maji kabla ya kunywa, hii ni baada ya wagonjwa wengi  kuenda hospitali wakiwa wameathirika  na  ugonjwa wa homa ya matumbo, ambao husababishwa na maji chafu.

“Naomba watu wote kuchemsha maji kabla ya kunywa ili kujiepusha na ugonjwa wa homa ya matumbo ambao umeshuhudiwa kutokana  na kunywa maji chafu,” alihoji Kingoina.

Aidha, amewaomba wakazi wote kuzingatia usafi haswa kunawa mikono kabla ya kula, na kuwahimiza wazazi na walimu kuwafunza watoto umuhimu wa kunawa mikono.

Kwingineko, mhudumu huyo amewashtumu wanaoshughulikia mifereji ya maji chafu katika mji wa Kisii na viunga vyake, na kusema kuwa kufuja kwa mifereji ya maji taka hiyo kumesababisha maji kuwa machafu katika mji wa Kisii.

“Mifereji nyingi imefuja na wakaazi wengi kutoka hapa Kisii hutumia maji kutoka mito ambayo mifereji hiyo uchukua uchafu huo hadi mito hiyo ambayo watu huchota maji hayo bila wao kujua kama yamechafuliwa kutoka kwingine,” aliongezea Kepha

Kwa sasa amewaomba wakazi kuchota maji mahali pasafi na kuyachemsha ili kujikinga na maradhi yanayosababishwa na maji chafu.