Kamishena wa kaunti ya kisii Chege Mwangi amesema uchumi wa kaunti hiyo utaimarika zaidi ikiwa utumizi wa dawa ya kulevya utapungua katika kaunti hiyo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza siku ya Ijumaa katika ofisi yake, kamishena huyo alisema visa vya utumizi wa dawa za kulevya vikipungua katika kaunti ya Kisii basi wakaazi wa kaunti hiyo watakuwa na kila sababu ya kutabasamu kwani uchumi utaimarika.

“Ikiwa dawa ya kulevya hayatatumiwa na vijana wetu wa kaunti hii, wakaazi wote kwa ujumla watavuna matunda ya kunawiri kwa maendeleo haswa ya kiuchumi,” alisema Mwangi.

Aidha, kamishena huyo alisema dawa za kulevya ni hasara kwa wanao tumia dawa hizo maana hawafaidiki na chochote.

Alisema kuwa ni sharti watu waweke kando utumizi huo wa dawa za kulevya na kujihusisha na maendeleo.

Matumizi ya dawa ya kulevya ni hatia katika serikali ya Kenya. Tunapaswa kuepukana na dawa hizo kabisa,” alisema Mwangi.

Hii ni baada ya kampeni ya kupambana na na utumizi wa dawa za kulevya  kufanyika katika Chuo Kikuu cha Kisii.

Chuo hicho kimekuwa kikishirikiana na tume ya kupambana na utumizi mbaya wa dawa hizo kwa siku tatu mfululizo.